Yoana Fransiska wa Chantal
Mandhari
Yoana Fransiska wa Chantal (kwa Kifaransa Jeanne-Françoise Frémiot, Baronne de Chantal; (Dijon, Burgundy, Ufaransa, 28 Januari 1572 – Moulins, 13 Desemba 1641) ni maarufu kwa kuanzisha na kuongoza kwa busara shirika la kitawa la wanawake la Ziara ya Bikira Maria baada ya kufiwa mumewe ambaye alizaliana naye watoto sita, aliowalea Kikristo sana.
Baada ya kubaki mjane alifuata kasi sana njia ya ukamilifu chini ya uongozi wa Fransisko wa Sales, akijitosa katika matendo ya huruma hasa kwa fukara na wagonjwa[1].
Papa Benedikto XIV alimtangaza mwenye heri tarehe 21 Novemba 1751, halafu Papa Klement XIII alimtangaza mtakatifu tarehe 16 Julai 1767.
Sikukuu yake imehamishiwa tarehe 12 Agosti[2] kutoka 12 Desemba.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- St. Jane Frances de Chantal Archived 2005-04-22 at the Library of Congress Web Archives at Saint of the Day
- The Life of Saint Jane Frances de Chantal Ilihifadhiwa 8 Agosti 2007 kwenye Wayback Machine.
- St. Jane Frances de Chantal at Catholic Online
- Saint Jeanne de Chantal Ilihifadhiwa 16 Juni 2008 kwenye Wayback Machine. at Patron Saints Index
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |