Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia ya Kituruki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wikipedia ya Kituruki

Wikipedia ya Kituruki (Kituruki: Türkçe Vikipedi) ni toleo la kamusi elezo huru ya Wikipedia kwa lugha ya Kituruki. Ilianzishwa mnamo mwezi wa Desemba 2002, na kwa tar. 3 Februari 2008, toleo hili lina makala zaidi ya 100,000.

Hii ni Wikipedia ya 17 kwa ukubwa wa hesabu ya wingi wa makala, na ni moja kati ya Wikipedia 16 yenye idadi ya milioni nne ya uhariri wa makala. Pia, ni moja kati ya Wikipedia 13 zenye zaidi ya watumiaji 150,000 waliojisajiri.

Mnamo mwezi wa Novemba katika mwaka wa 2006, Wikipedia ya Kituruki imeteuliwa chini ya kundi la Sayansi kwa ajili Altın Örümcek Web Ödülleri (Golden Spider Web Awards), ambayo inajulikana sana kama "Web Oscars" for Turkey.[1] Mnamo mwezi wa Januari 2007, Wikipedia ya Kituruki imepewa tuzo kwa kuwa na makala bora. Tuzo hiyo ilitolewa wakati wa sherehe mnamo tar. 25 Januari 2007 katika Chuo Kukuu cha Ufundi cha Istanbul.

Na kwa mwezi wa Mei 2009, Wikipedia ya Kituruki imekuwa ya pili kwa ukuaji wa Wikipedia zenye makala zaidi ya 100,000.

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-28. Iliwekwa mnamo 2009-05-07.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikipedia
Wikipedia
Wikipedia ya Kituruki ni toleo la Wikipedia, kamusi elezo huru
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wikipedia ya Kituruki kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.