Pierre Borie
Pierre-Rose-Ursule Dumoulin-Borie (20 Februari 1808 – 24 Novemba 1838) alikuwa padri Mkatoliki wa Ufaransa aliyefanya kazi kama mmisionari wa Paris Foreign Missions Society huko Vietnam hadi alipokatwa kichwa katika dhuluma ya kaisari Minh Mang [1].
Papa Leo XIII alimtangaza mwenye heri tarehe 27 Mei 1900, halafu Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu tarehe 19 Juni 1988 katika kundi la Wafiadini wa Vietnam.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 24 Novemba[2].
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Kisha kujiunga na seminari ya Servières mwaka 1824, alipata upadrisho huko Bayeux tarehe 21 Novemba 1830 akatumwa ng'ambo, akifikia Macao tarehe 18 Julai 1831.
Akikwepa vizuizi vya serikali dhidi ya umisionari, alifaulu kufikia Saigon na kujiunga na misheni ya Tonkin Kusini (Vietnam).
Bila kujali dhuluma ya serikali, alidumu kutekeleza majukumu yake ya kichungaji katika eneo alilokabidhiwa mpaka alipokamatwa mwaka 1838.
Akiwa gerezani, alipata taarifa ya kuwa ameteuliwa kuwa askofu tangu tarehe 30 Januari 1836.
Muda mfupi baadaye, tarehe 24 Novemba 1838, aliambiwa amehukumiwa adhabu ya kifo akauawa siku hiyohiyo pamoja na mapadri wenzake Petro Vo Bang Khoa (1790 - 1838) na Vinsenti Nguyen The Diem (1761 - 1838).
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- "Pierre-Rose-Ursule-Dumoulin Borie". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913. http://www.newadvent.org/cathen/02686c.htm.
- (Kifaransa) Saint Pierre Dumoulin-Borie at Missions Etrangères de Paris
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- (Kifaransa) Archives of the Paris Foreign Missions Society Ilihifadhiwa 5 Desemba 2014 kwenye Wayback Machine.
- Catholic Hierarchy
- https://web.archive.org/web/20141226035930/http://www.gpnt.net/diendan/archive/index.php/t-1167.html
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |