Aden Elly’s Post

View profile for Aden Elly, graphic

Expert in Community-Based Humanitarian Initiatives | Driving Impact Through M&E, Stakeholder Engagement, Community Protection and Financial Precision

Am reposting my post with this LinkedIn translation, for me it is somehow sounding interesting. How would you rate this translation?

View profile for Aden Elly, graphic

Expert in Community-Based Humanitarian Initiatives | Driving Impact Through M&E, Stakeholder Engagement, Community Protection and Financial Precision

Kwenye maisha haya kila jambo linawezekena. kikubwa unachotakiwa kufanya hakikisha haupotezi focus yako. Mazingira yanaweza kuwa magumu kiasi yakwamba hauoni njia ya kutokea, lakini wewe endelea kupambana hadi hatua ya mwisho. Wakati mwingine inawezekana mafanikio yako yamewekwa kwenye chumba cha 99, hivyo usiishie chumba cha 80 ukakata tamaa kwamba umeshatembea vyumba vingi na bado hujaona matokeo. Wewe komaa mpaka chumba cha mwisho, ili uwe na uhakika kama hakuna, hakuna, kama ipo itakuwepo. Kwani haukumbuki habari za wale wakoma wanne walioandikwa kwenye kitabu cha Wafalme wa pili sura ya sita? Wao walikuwa na njaa, na mahali pekee wangeweza kupata chakula ili wale washibe ilikuwa kwa jeshi la washami. Sasa wanaulizana je? twende ili kama wakituua basi tufe tu au wakituacha hai basi tutakuwa hai na tutakula chakula au tubakie hapa tufe na njaa, Jamaa wakaamua kulifuata jeshi la wa shami hukohuko waliko pamoja na udhaifu wao wa kuwa wakoma, sasa Mungu alivyo waajabu akatia vishindo vikubwa kwenye miguu ya wakoma mpaka jeshi la washami wakaogopa wakatimua mbio na wakoma wakapata msosi, Wakala na kusaza na wakawaita na wenzao waje kukusanya chakula wale maana walikuwa na njaa kwani hawakuwa na chakula. Kwahiyo basi, chochote unachokifanya cha kuleta maendeleo, usiogope changamoto, wewe songa mbele, kwani ushindi wako upo karibu na Bwana atakufanyia njia pasipo na njia. Nani angetegemea kama Timu ya Young African Club Jana ingeweza kushinda kombe la #CRDB? ilikuwa heka heka na kivumbi, mpaka matuta yakaisha na kuongezwa lakini mwishoooni wakatwaa ushindi. #Don't #give #up you still have an #opportunity to change the situation

To view or add a comment, sign in

Explore topics